Uzinduzi wa mafunzo kazini kwa walimu mradi wa EQSSE-Z
Shirika la Good Neighbors Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Linatarjia kufanya Uzinduzi rasmi wa Mafunzo kazini kwa Walimu na kukabidhi Moduli na Miongozo ya mafunzo.
Hafla hii itafanyika Siku ya tar 3 Agosti 2022 katika hoteli Golden Tulip Zanzibar Airport.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Hussein Ali Mwinyi atakuwa mgeni Rasmi.
Viongozi mbali mbali wakiwemo Mawaziri, Manaibu Waziri Makatibu wakuu wa Wizara, Mabalozi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya watahudhuria.
Kupitia Hafla hii Shirika la Good Neighbors Tanzania litakabidhi Moduli na miongozo itakayotumika katika mafunzo wa Walimu wa masomo ya Hisabati, Sayansi na Kiingereza pamoja na Kamati za Skuli..ambayo yana lengo la Kuimarisha ubora wa Elimu ya Sekondari Zanzibar.